Habari ziko sky news sasa kuwa ndege ya Malaysian airways imeanguka ikiwa na abiria 295
Kuanguka kwa ndege ya Malaysia si ajali,bali shambulio la kigaidi yasema Ukraine
Hii ni ndege ya pili sasa
Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria
iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa
hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi
vya serikali.
Wanasema abiria wote 298 waliokuwa katika ndege
hiyo ya shirika la Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam
kuelekea Kualar Lumpur wameufariki.
Wengi wa abiria hao walikuwa ni raia wa Uholanzi.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi.
Maafisa wa Ukraine walichapisha kile walichotaja
kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza maafisa
wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ukraine,
Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidi wa kutosha kwamba
ndege hiyo ilidunguliwa.
' Tulinasa pia mawasiliano ya simu kati ya magaidi hao wakizungumzia kundunguliwa kwa ndege hiyo.
Kwa sasa tunatafsiri sauti zao na kisha tutaziweka kwenye mtandao wa internet ili kuthibitisha hilo."
Hata hivyo sauti hizo zilizonaswa bado
hazijathibitishwa na upande uliohuru na waasi hao wamekanusha kuhusika
wakisema kuwa ni wanajeshi wa serikali ndio walioidungua ndege hiyo.
Kadhalika marekani imesema kuwa inaamini ndege hiyo ililipuliwa angani na wala halikuwa tukio la ajali.
Makamu wa rais Joe Biden hata hivyo amesisitiza kuwa Marekani bado inatafuta maelezo.
''Ndege ya Malaysia iliyokuwa ikitoka Ulaya
magharibi kuelekea Kuala Lumpur, yaelekea ilipokuwa ikivuka karibu na
mpaka kati ya Ukraine na Urusi, nasema yaelekea kwa sababu hatuna
taarifa za kina, nataka kuwa makini na kile ninachosema yaelekea
ilidunguliwa, ilidunguliwa na wala sio ajali. Ililipuliwa kutoka angani.
Tunaona ripoti kwamba huenda raia wa Marekani walikuwa kwenye ndege
hiyo na bila shaka huo ndio wasiwasi wetu wa kwanza.''
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kuwa Ukraine inapaswa kuwajibika katika tukio la udunguaji wa ndege hiyo.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema kuwa mkasa
huo haungetokea ikiwa Kiev haingeimarisha harakati zake za kijeshi
mashariki mwa Ukraine.
=====
Smoke rising: Flight from Amsterdam which crashed in Donetsk
A Malaysia Airlines plane has crashed in Ukraine with 295 people on board.
Reports this afternoon say the passenger jet was travelling from Amsterdam to Kuala Lumpur, and is thought to have crashed near to the Russian border.
The Russian Aviation Industry said the plane did not enter Russian airspace when expected, but crashed in Eastern Ukraine.
It comes just over four months after the airline's Flight MH370 disappeared without trace as it flew from Kuala Lumpur to Beijing
The Interfax report said the plane came down 50km (20 miles) short of entering Russian airspace.
An unnamed source said it "began to drop, afterwards it was found burning on the ground on Ukrainian territory."
The plane appeared to have come down in a region of military action where Ukrainian government forces are battling pro-Russian separatists.
A separate unnamed source in the Ukrainian security apparatus, quoted by Interfax, said the plane disappeared from radar at a height of 10,000 metres after which it came down near the town of Shakhtyorsk.
The Ukrainian Interior Ministry says the plane was brought down by a ground-to-air missile.
280 passengers were on board, with 15 crew. All are believed to have died.
Malaysia Airlines has confirmed it has lost contact with flight MH17 from Amsterdam.
One Ukrainian official claims MH17 was shot down by a missile fired from a Buk launcher, while flying at an altitude of 33,000ft.
The footage below shows the type of missile launcher they say was involved.
Russia Today has tweeted this picture, which they say is an eyewitness photo of debris where MH17 came down.
The image has not yet been verified.
Chanzo:mirror & BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment