Mfano wa Sarafu ya 500 kama iliyoonekana katika Banda la Benki Kuu katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Hii ni Baada ya noti ya shilingi mia tano kuwa kwenye mzunguko mkubwa hivyo kuchakaa mapema,benki kuu ya Tanzania imeamua kuleta sarafu ya shilingi miatano mwaka huu wa fedha inayotamiwa kudumu kwa miaka zaidi ya ishirini
sarafu ya shilingi mia Tano inatarajiwa kuzinduliwa na Benki Kuu ya Tanzania. Sarafu hiyo itatumika sambamba na noti za shilingi mia Tano huku zikiwa zinaondolewa taratibu. Hayo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki na Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emanuel Boaz.
Noti ya shilingi mia tano |
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza mchakato wa kufanyia mabadiliko ya noti mpya ya Sh500, ili iwe ya sarafu baada ya kujiridhisha kuwa inachakaa kwa haraka zaidi.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, alisema mchakato kuifanyia mabadiliko na noti hiyo ili iwe katika sarafu, inazingatia ukweli kwamba fedha iliyoko katika mzunguko mkubwa katika jamii.
Profesa Ndulu alisema noti ya Sh500 inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi wengi, jambo linalosababisha kuchakaa haraka kabla ya wakati uliopangwa.
“Tunafanya mchakato wa mabadiliko ya noti hizi zinazochakaa kwa haraka kwa sababu zenyewe zinatumika zaidi,” alisema Profesa Ndulu.
Alisema hatua hiyo haitaathiri mzunguko wa fedha na kwamba sarafu ya Sh500 itakapoanza kutumika, noti hiyo itaondoka polepole.
Alisema sarafu hiyo ya Sh 500 itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho na kuwawezesha wananchi kuitumia.
“Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji,”alisema
No comments:
Post a Comment