Wednesday, 2 July 2014

HABARI ZA UMBEYA/ NDOA YA DIDA YAVUNJIKA TENA

Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe, Ezden Jumanne siku ya harusi yao.




Baada ya ndoa ya Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu 'Dida' kudaiwa kuvunjika, mumewe anayepiga mzigo TV1, Ezden Jumanne amefunguka mengi kuhusu sababu za kuvunjika ndoa hiyo.


‘Dida’ na Bw. Ezden wakati wa harusi yao.
Alisema siku moja mtalaka wake huyo alimweleza kuwa kuna rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Furaha amempa mchongo wa kuwa mgeni staa (celebrity guest) ndani ya Jumba la Big Brother na kumuomba ampe ridhaa ya kwenda huko.Akizidi kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Risasi Mchanganyiko, Ezden alisema: 
“Nilimruhusu kwa moyo mmoja ambapo pia aliniomba nimsaidie kumpa uzoefu juu ya lugha ya Kiingereza ili akaendane na kanuni za Big Brother.

Ezden akipozi.
“Kama mume nilimsapoti kwa nguvu zote, siku nyingine kama nikiwa nimerudi nyumbani mapema mimi mwenyewe nilikuwa nikimfundisha ‘tense’ mbalimbali.”

Katika aya nyingine, Ezden alisema kuna siku Dida alimfungukia kuwa hatakwenda Big Brother kama mgeni staa kwani anatakiwa kuingia kama mshiriki na kumwambia kuwa alikuwa akiogopa kumwambia ukweli mapema.

“Nilimkatalia ndipo alipocharuka, huwezi amini alifikia hatua  ya kusema nambania zali lake. Niliumia sana siku ile ikabidi nimuulize kama anaithamini Big Brother kuliko ndoa yake, hakunijibu.

“Kama mume ilibidi niwaulize wazazi na mashemeji zangu kama wamemruhusu Dida kushiriki shindano hilo kama alivyoniambia, walidai aliwaambia kuwa mimi ndiye niliyemruhusu ndiyo maana nao hawakuwa na pingamizi.

'Dida' akiwa ofisi za Times FM.
“Baada ya kuwaelewesha waliniambia hawakupenda mambo hayo ya Big Brother kwa kuwa yana udhalilishaji ndani yake,” alisema Ezden.

Siku ya tukio, Ezden alisema alikuwa akioga bafuni na simu yake ilikuwa kitandani, ghafla Dida alimfuata na kumuuliza kwa nini aliweka password! 

“Alipiga kelele mpaka majirani wakaanza kujaa nyumbani kisa ‘password’ niliyoiweka kwenye simu yangu. Nikamuuliza yeye si ndiye aliyesema kuwa kila mtu awe na simu yake! Akaanza kunipa maneno ya kejeli.

“Hapo nikaona heshima yangu inashuka. Kiukweli nilimpiga mpaka nikamuumiza. Baadaye akaondoka kwa hasira kumbe alikwenda kuwachukua ndugu zake.

“Walipokuja tukajitahidi kusuluhisha lakini kila nilipopewa nafasi ya kuzungumza, Dida aliniingilia. Kwa kuwa tulishawahi kukaa vikao vingi sana kabla lakini hakuna tulichoweza kusuluhisha, niliona hakuna  haja ya kuendelea naye,” alisema Ezden na kuongeza kuwa kikao hicho kiliisha kwa ahadi kwamba angetoa talaka kwa Dida ambaye naye alionekana kuikubali.



Ezden alisema, Juni 28, mwaka huu  alimpa Dida talaka tatu na kuongeza kuwa hategemei kurudiana naye wala kuoa hivi karibuni.Kwa upande wake, Dida alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema: “Mimi sina la kusema na wala sitaki kulumbana na mtu.”
CRD. MATUKIO NA VIJANA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!