UVUMI kwamba mwigizaji Lucy Komba kuwa katika mahusiano na mzungu kutoka nchini Denmark, zimedhihirika kuwa ni kweli baada ya wawili hao kupanga kufunga ndoa Septemba mwaka huu.
Lucy, muongozaji, mtunzi na muongozaji wa filamu wa siku nyingi, aliihakikishia Ijumaa wikienda kuwa kwa sasa yupo katika maandalizi ya harusi yake hiyo ambayo anatarajia kuifanyia hapa nchini na tayari kashanza kugawa kadi.
Hata hivyo, alipotakiwa kutaja jina kamili la mwandani wake huyo alikataa na kumtaja kwa jina moja la Stanley kwa madai anaogopa wasanii wenzie wasije wakamfanyia zengwe.
No comments:
Post a Comment