Zaidi ya Maofisa kutoka wizara tatu wapato 13 waliokuwa wakifanya kazi katika uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere, wamerudishwa katika wizara zao kwa kosa la kupokea rushwa kwa wageni wanaoingia kutoka nchi mbalimbali.Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Uchukuzi Dr. Herrison Mwakyembe alisema kuwa, maofisa hao walikuwa katika kitego cha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Afya na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.Wageni ambao walikuwa wanakaguliwa na kuobwa rushwa na wafanyakazi hao ni kutoka nchini China, India na Nchi za Kiarabu, ambao wakifika uwanjani hapo wanakaguliwa mabegi kama amebeba dawa za asili dawa hizo huchukuliwa na maofisa wa kilimo na baadae kuobwa pesa na kurudishiwa dawa hizo.
Pia kama ameingia hajachoma sindano ya homa ya manjano anaamriwa na kuulizwa kwanini hujachoma na akioneakana anakaidi anaambiwa atowe chochote kitu kisha anaachiwa, hivyo hivyo kwa upande wa uvuvi na mifugo nako wanafanyiwa hivyo.
No comments:
Post a Comment