Pages

Friday, 25 July 2014

ALLI KIBA SINA BIFU NA DIAMOND

STAA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Alikiba amekanusha kwamba ana ugomvi na nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ kama ilivyokuwa ikifahamika na wadau wengi wa muziki huo.

Akizungumza katika kipindi cha Sporah Show kinachorushwa na Clouds TV, alisema hana ugomvi na msanii yeyote kwani anajitambua na hawezi kuendeleza chuki na wasanii wenzie.
“Diamond aliwahi kunikosea sana, lakini mimi kwa sababu sio mtu wa kukasirikika niliamua kuachana nae na kufanya yangu, lakini nashangaa kila kukicha nasoma kwenye vyombo vya habari kwamba nilimkosea, lakini kiukweli sina ugomvi na mtu.
“Katika wimbo wake wa ‘Lala salama’, kuna sehemu niliweka vionjo vyangu baada ya kunitaka nifanye hivyo, lakini cha kushangaza baada ya wimbo kutoka sikusikia sauti yangu ila nilipoimba mimi akaimba yeye, kiukweli nilijisikia vibaya, lakini nikaachana na hayo,” alisema.
Alikiba alisema maadamu anapenda muziki tena akiwa mpenzi wa nyimbo za Diamond, anampongeza kwa mafanikio makubwa aliyopiga hadi kuing’arisha nchi kimataifa ikiwamo katika tuzo mbalimbali.
Alikiba ametamba na ngoma zake kama, ‘Dushelele’, ‘Cindelera’, ‘Mali yangu’, ‘My Everything’, ‘Single Boy’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

No comments:

Post a Comment