Friday, 27 June 2014

YULE CHATU ALIYERIPOTIWA KUONEKANA MAENEO YA SINZA HABARI YA KUWEPO KWAKE NI HII..

Dar: Wezi waiba begi lenye chatu wakidhani pesa


Mwenye nia mbaya anaweza kudhani amepata kumbe amepatikana, anaweza ukadhani kila siku atapiga bingo kama hatakamatwa na raia kumbe mzigo alioiba unaweza kugeuka fimbo na hatari kubwa kwake hata bila kukamatwa.

Watu wasiojulikana wanasadikika kuiba begi kubwa maeneo ya Sinza, Dar es Salaam wakidhani begi hilo lina pesa na badala yake wakakutana na chatu mkubwa walipolifungua.

Wakazi wa Sinza walimkuta chatu huyo katika daraja akiwa karibu na sanduku hilo linaloaminika kuwa lilimbeba chatu huyo. Inaelezwa kuwa wezi hao walilitupa begi hilo na kutokomea pasipojulikana baada ya kuona mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!