Tuesday 10 June 2014

WANANCHI WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU

WANANCHI wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari, ili taifa liweze kuwa na akiba ya kutosha na lifikie malengo ya maendeleo ya milenia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alisema malengo ya milenia pia ni kuboresha afya ya mama na mtoto na kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua.
Alisema kutokana na mahitaji ya damu kuwa makubwa kuliko upatikanaji, baadhi ya ndugu hulazimika kuchangia damu pale inapokosekana, ili kunusuru maisha ya ndugu yao.
“Inakadiriwa mahitaji ya damu kwa mwaka ni wastani wa chupa 400,000 mpaka 450,000, kwa sasa uwezo wa mpango unakusanya kati ya chupa 150,000 kwa mwaka, hali inayosababisha vifo vingi kutokea kutokana na upungufu huo,” alisema Dk. Rashid.
Alisema juhudi mbalimbali zinaendelea kufanywa na serikali, ili kuongeza makusanyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vidogo vya usambazaji na ukusanyaji damu katika mikoa.
“Serikali imeanza kufanya jitihada mbalimbali kukabiliana na tatizo hili, hadi sasa vipo vituo vidogo vimeanzishwa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Lindi, Morogoro na Dodoma,” alisema.
Awali, Meneja Miradi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk. Efesper Nkya, alisema uelewa mdogo wa wananchi katika suala la kuchangia damu umechangia malengo ya milenia kushindwa kufikiwa kwa wakati.
TZ-DAIMA


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!