Tuhuma za Beyonce kumsaliti Jay Z na kutoka na mlinzi wake aitwae Julius De Boer zilisambaa mwezi uliopita huku likiwaacha mashabiki wao midomo wazi.(kamailikuputa Bonyeza HAPA)
Katika hali inayoonekana kuwa Jay Z amezifanyia kazi kwa msisitizo zaidi, Beyonce ameonekana mitaani akiwa mlinzi mwingine ambaye hakufahamika huku wengi wakiuliza nini kimemkuta Julius? Au ndio katimuliwa kabisa?
Taarifa za awali zilidai kuwa Jay Z baada ya kuona Julius yuko karibu sana na Beyonce huku ikielezwa kuwa mara nyingi waliposafiri pamoja kwenda ziarani, walikaa hotel moja na mlinzi huyo alikuwa anaingia hata chumbani kwake.
Inadaiwa kuwa Jay Z aliamua kumfukuza kazi Julius lakini Beyonce aliweka ngumu
Wanandoa mastaa, Beyonce Knowles na Jay Z wamekuwa wakihudhuria sherehe mbalimbali licha ya kuwepo uvumi kuwa ndoa yao ipo matatani lakini tetesi hii inaweza kuwa kubwa zaidi kuwahi kusemwa.
Beyonce akiwa na bodyguard wake, Julius
Kuna tetesi kuwa Beyonce amekuwa akimsaliti mumewe na kutembea na bodyguard wake Julius De Boer.
Beyonce anadaiwa kuwa karibu mno na Julius De Boer, mzaliwa wa Uholanzi ambaye amekuwa akimlinda tangu mwaka 2009. Habari zimedai kuwa Jay Z ana wasiwasi pia na uhusiano wao.
“Jay kiukweli anahisi kuwa kunaweza kuwa na kitu cha kimahaba kinaendelea kati ya Bey na Julius,” chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Mstarz News. “He wanted to fire Julius last February, but Beyoncé said, ‘Julius isn’t going anywhere. They’ve spent a lot of time together behind closed doors. He’s even stayed in her hotel room.”
Kumekuwepo na tetesi za wawili hao kupeana talaka japo wamekuwa wakiikwepa. Tukio la Jay Z na Solanga kugombana kwenye lifti hivi karibuni liliongozea nguvu tetesi hizo.
No comments:
Post a Comment