Monday 9 June 2014

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/25 07 Juni, 2014
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango, Geological Survey of Tanzania

(GST) na Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na
Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), anatarajia kuendesha
usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi
watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanywa kabla ya usaili kuanza.
2. Usaili wa ana kwa ana utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na
utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Wafike na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Wafike na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha
nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za
matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kila msailiwa azingatie muda, tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa
usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth
Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena
mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
12. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo
wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa
kwenye tangazo.

DOWNLOAD MAJINA HAPA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!