Mzee Small ni miongoni mwa waigizaji wakongwe nchini ambao kupitia kazi yake ya sanaa ya maigizo ndani na nje ya Tanzania tulimtambua usiku wa June 07 zilianza kusambaa taarifa za kifo chake.
Ingawa kama unakumbuka December 10 2013 Mzee Small pia aliwahi kuzushiwa kifo na familia ikasema ile ilikua ni mara ya pili kwa Mzee Small kuzushiwa kufariki dunia.
Muhidin ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Small amethibitisha kifo cha Mzee Small na kusema ni kweli kafariki na amefariki akiwa anapata matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili Dar es salaam mpaka sasa sababu za kifo chake zimesemwa kuwa ni presha baada ya kuugua kwa muda mrefu.
ENDELEA KUWA NASI KWA HABARI KAMILI KUHUSU HABARI HIZI ZA KUHUZUNISHA..
CHANZO: MILLARD AYO.COM
No comments:
Post a Comment