
Tuuenzi mwezi huu mtukufu kwa kufanya yale yaliyo mema, na pia tusiwasahau wale wote ambao mungu hakuweza kuwajaalia kwa hali moja au nyingine, kama watoto yatima, watoto wa mitaani wagonjwa n.k. kwa ushauri wa bure tu: watu wengi mwezi huu hualikana mialiko mbalimbali ya kufuturu pamoja, nimeona wengi wanaalika watu maarufu, au mtu ambaye tayari amejitosheleza, nivyema zaidi ukaalika yule ambaye anahitaji sanasana msaada wako, watoto wa mitaani , mayatima, wagonjwa, na kwa kweli watu kama hao tunao wengi ambao wangekushukuru sana kwa kile kidogo ulichowakumbuka..
TUNAWATAKIA RAMADHANI KAREEM!
No comments:
Post a Comment