Tuesday, 24 June 2014

RAIS KIKWETE AAPISHA BALOZI MMOJA NA WAJUMBE WANNE WA TUME YA OPERESHENI TOKOMEZA


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Balozi aliyeapishwa ni Mhe. oseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi,Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela. Pichani Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo,kupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. akimkabidhi Balozi Joseph Edward Sokoine  miongozo ya kazi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. akimpongeza Balozi Joseph Edward Sokoine
Wajumbe wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal(Wanne Kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kulia) wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo Bwana Frederick Kapela Manyanda, Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo(wapili kushoto), Jaji mstaafu Hamisi Amiri Msumi(Watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema(kulia),Wasita kushoto ni  Balozi Joseph Edward Sokoine. Picha na Freddy Maro
chanzo:jiachie blog

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!