Maisha ni magumu Brazil linapokuja suala la mawasiliano na sasa nimeajiri Mkalimani wangu. Kijana mmoja Mtanzania anaitwa Tuli ambaye ni mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam na anafahamu vyema lugha ya Kireno.
Alikuja hapa kwa ajili ya shughuli zake, lakini ameambulia kuifahamu vizuri lugha hii. Kwa wageni tuliopo hapa, unalazimika kutembea na mkalimani kama hauifahamu Lugha ya Kireno.
Hii ndiyo lugha pekee ambayo inatamba Brazil. Wenye nafuu ya kusikilizana na hawa Wabrazil wanabakia kuwa Wahispaniola na wakazi wengine wa Amerika Kusini.
Wahispaniola lugha yao inaingiliana na Kireno. Lakini Kiingereza na Kiswahili changu ni lugha zisizo na mteja kabisa ndani ya mitaa ya Sao Paolo. Unaweza kuagiza sukari ukaletewa Ndimu na mchuzi.
Wahudumu wengi katika baa mbalimbali kwa sasa wanatumia mbinu ya kushika peni na karatasi kwa ajili ya kumchorea mteja kitu anachohitaji. Bahati nzuri wanatambua kuwa wageni wengi waliokuja katika michuano ya kombe la dunia hawajui Kireno.
Nilishuhudia tatizo hili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Sao Paolo nilipofika. Jamaa wa Uhamiaji aliyenihudumia hawezi kuongea Lugha ya Kiingereza na wala hakuwa na mpango wa kuniuliza maswali yoyote zaidi ya kuangalia uhalali wa visa yangu
Nilishuhudia tatizo hili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Sao Paolo nilipofika. Jamaa wa Uhamiaji aliyenihudumia hawezi kuongea Lugha ya Kiingereza na wala hakuwa na mpango wa kuniuliza maswali yoyote zaidi ya kuangalia uhalali wa visa yangu.
No comments:
Post a Comment