Hii imenisiktisha sana na ndio maana nimeileta humu kwa blog, ili kila mtu aelewe,kwanini Watanzania tunakosa ustaarabu, ukishatukana au kuweka picha za matusi mitandaoni, unapata faida gani? wengi wanatumia mitandao kwa vitu vya kijinga, badala ya kuandika vitu vya maana na vyenye manufaa kwko na kwa jamii, HII INAONYESHA JINSI GANI TUKO NYUMA KIMAENDELEO,
Siku za nyuma kunablog moja imetoa picha za matuzi za Michelle Obama, nakumdhalilisha mwanamke wa watu, haya sasa hivi ni Fashion blog nyingi ni Picha za matusi tu, hii tabia inanikerasana! kumbukeni kwamba hilo ni kosa la jinai, kunadi picha au maisha ya mtu mwingine bila ridhaa yake, halafu unaona kama ni ufahari! sasa sheria inakuja, na nina imani itawabana tu, ukionekana unamuandika mtu bila ridhaa yake, unatupwa lupango, na faini juu, kijiblog chako kinafungiwa,nasubiri sana hiyo sheria, kwanini umnyime mwenzio raha,kwa faida zako wewe? watu wamefikia kutengeneza picha za matusi na kuzitangaza mitandaoni, sasa leo nakumbana na hii ya mama Wema Sepetu, maskini mama wa watu amewakosea nini? yaani kweli mmekosa heshima kiasi hicho! Ni ushamba Acheni bwana, kuwa mstaarabu hakukugharimu chochote..
No comments:
Post a Comment