Thursday 5 June 2014

MWAKYEMBE KUONGEZA NDEGE ATCL

Mwakyembe kuongeza ndege ATCL
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameahidi kuongeza idadi ya ndege iwapo deni kubwa linalolikabili Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) litalipwa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi, muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Uholanzi, waziri huyo alikiri kuwepo kwa mzigo wa madeni ATCL.
“Ushirikiano wetu ulianza mwaka 1978 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati ule tulikuwa vizuri kwenye sekta ya anga.
“Mashirika mawili yalikuwa yakiruka, ATCL na KLM, tena mara saba kwa wiki, mwaka 1998 tulirekebisha na kuongeza baadhi ya maeneo ikiwemo kuongeza idadi ya mashirika ya ndege, siku za kuruka na vituo,” alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema licha ya kukosa ndege za kutosha na madeni yanayoikabili ATCL, serikali inaruhusu wawekezaji binafsi kusajili makampuni na ndege zao hapa nchini.
“Tunadaiwa sana ATCL, lakini tukisafishiwa mizania nina uhakika sekta ya anga itapaa na tutanunua ndege za kutosha,” alisisitiza waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Kyela.
Balozi wa Uholanzi aliyesaini mkataba huo kwa niaba ya nchi yake, Jaap Frederiks, alisema Tanzania ni nchi yenye kila sababu ya kuwekeza.
TZ-DAIMA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!