Thursday, 19 June 2014

MUME WA FLORA MBASHA APEWA DHAMANA

Mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akipelekwa mahabusu ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar.

...Emmanuel Mbasha akifungiwa ndani ya mahabusu.
...Askari Magereza akifunga mlango wa mahabusu.
...Emmanuel Mbasha akielekea kizimbani.
MUME wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) anayekabiliwa na kesi ya ubakaji amepewa dhamana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar baada ya kutimiza masharti.
Mbasha amefikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Keko alikopelekwa Juni 17 mwaka huu akikabiliwa na kesi ya kumbaka shemeji yake.
Mbasha baada ya kutolewa kwenye mahabusu ndogo ya mahakamani hapo alionekana mnyonge na aliyechoka hali iliyosababisha simanzi kwa ndugu na jamaa zake waliokusanyika mahakamani hapo.
Baada ya kesi hiyo kutajwa, rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa mtuhumiwa huyo, Mwahimu Juma walifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!