Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro DKT Godfrey Mtei akilia kwa uchungu!
Mwili wa marehemu ukipelekwa jukwa kuu
Mkuu wa Mkoa Joel Bendera[mwenye suti] akiwasili Uwanja wa Jamhuri
Bibi Asha Abdallah ambaye ni bibi wa mtoto Nasra akihojiwa na waandishi wa habari Uwanjani hapo
Baada ya kupigwa maswali magumu na waandishi hao Bibi huyo alishwa na kujibu na kuangua kilio
Nasoro Mahamba ambaye anazaliwa tumbo moja na Nasra kwa mara ya kwanza ameibuka Uwanja wa Jamhuri Kuaga mwili wa mdogo wake,lnadai Nasoro baada ya mateso aliyoyapata kutoka kwa mama yake mkubwa aliamu kutoroka na kwenda kumtafuta baba yake ambaye alifanikiwa kumuona maeneo ya Kihonda anakoishia kwa sasa.Marehmu Nasra alishwa kuwakimbia mateso hayo kama alivyofanya kaka yake kufuati umri wake kuwa mdogo.
Nasoro akihojiwa na Mtandao huu
Nasoro akipokea shilingi elfu kumi kutoka kwa mmoja wa wasamilia wema
Mkuu wa mkoa Joel Bendera akimsalimia bibi wa marehemu Nasra
Jeneza la Nasra likiwa mbele ya viongozi wa serikali na dini
Askari wa dawati la Jinsia na maafisa wa Ustawi wa Jamii ambao ndio waliobeba jukumu la kumzika Nasra wakishuka kwenye gari na mwili wa marehmu
Bi,Amina Kingalu anayefanya kazi ya Omba Omba barabra ya madaraka akishiriki zoezi la kuaga mwili wa Nasra
Bi Josephine Joel [kushoto] ambaye alijitolea kumuuguza Nasra baada ya ndugu wa mtoto huyo kuingia mitini akiwa na bibi wa damu wa Nasra Asha Abdallah
Mkuu wa mkoa akizungumza na umati huo
Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini ambaye alilazimika kuacha vikao vya bunge kuja jimboni mwake kushirki zoezi la kuaga mwili wa Nasra akizungumza kwenye hafra hiyo
Sheikh wa Msikiti Mkuu wa Manispaa ya Morogoro Ally Omar akisoma dua la kumuombe marehmu,kwa sheria ya dini ya kiislam hakuna kipindele cha kuaga mwili wa marehmu hivyo Sheikh huyo aliwataka watu wa dini zote kusimama na kufuatila dua hilo na kwamba baada ya kukamilika kwa dua mwili ulipelekwa Msikiti mkuu kwa sara na baadae kuzikwa makaburi ya Kolla
Katika hali ya kuhudhunisha Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Godfrey Mtei aliangua kilio wakati wasifu wa Nasra uliposomwa, kulia kwa Dkt mtei ni baba mzazi wa Nasra Rashid Mvungi,Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Moro,Oswad Ngugamtitu,mkuu wa Mkoa Joel Bendara na Sheikh Ally Omar anayeonekana kwa mbali ni mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma
Baba wa Nasra akipokea Duwa
Viongozi wa serikali,siana na dini pamoja na mzazi wa marehmu Nasra
Ama kwa hakika kama kuna mtu anastahili pongezi ni huyu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Azimio Bi,Tatu Mgagalana ambaye baada ya kupokea taarifa za mateso ya Nasra aliyekuwa akishi mtaani kwake aliwaamulu wananchi wake kuvamia nyumba na Bi,Mariam na kumfichua Nasra aliyekuwa ndani ya boksi kwa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment