Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa anaishi kwenye boksi.
Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki kutokana na ugonjwa wa pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira machafu, kutoogeshwa na kupigwa na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika waliokuwa wakimfanyia ukatili huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kula njama za kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia na asiyeweza kujitetea, mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha masitaka ya kesi na kuwa KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.
Adhabu kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo, wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani hawa wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea kitanzi ili liwe fundisho kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama kawa hawa wendawazimu.
NIONAVYO:
Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi waonapo ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria ichukue mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba hatujaliani. Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa kimya. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au kunyanayaswa. Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu wanaoonewa bila sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile. Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake, liwe fundisho kwa watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na wanyonge.
No comments:
Post a Comment