Kwa mujibu wa mashuhuda kadhaa ambao walikuwepo tangu moto huo unawaka wamesema kuwa chanzo cha moto huo bado hawajajua ingawa wana wasiwasi na shoti ya umeme ambayo ilijitokeza usiku wa June 10.
Moto ulianza kuwaka saa 4 usiku ambapo iliwachukua zaidi ya saa moja kikoasi cha zima moto na uokoaji kufika eneo la tukio,baadhi ya Wafanyabiashara ambao bidhaa zao nazo zimeteketea wamesema kuwa hasara waliyoipata haielezeki kwani wengine wameshindwa kuokoa hata kitu kimoja.
Soko la Karume ni miongoni mwa masoko yanayotumiwa na wakazi wengi wa Dar es salaam na wale walio nje ya Dar es salaam kwa urahisi wa bidhaa zinazopatikana hapo,hizi ni picha za asubuhi ya June 11.
Picha zote kwa hisani ya Millard Ayo.com
No comments:
Post a Comment