Saturday, 7 June 2014

HABARI ZA UMBEYA/ HATIMAYE VICKY KAMATA AFUNGUKA KUHUSU NDOA YAKE ILIYOSHINDIKA



Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa mwanaume aliyetaka kufunga naye ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni habari za kutungwa na hazikuwa na ukweli wowote.

Vicky ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofungwa yalikuwa yametengenezwa na watu.
Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na hayo mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa hajaruhusu kuwa tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.

“Mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga vinginevyo , kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya binadamu.

“Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka 2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.

“Kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest zao ,lakini siyo kwamba nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu hata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu aliongea na vyombo vya habari akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi.

“Kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.
“Kuhusu kwamba hajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana, yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi.

“Hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini mungu ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu mwingine hataki bado ingefungwa…

“Kwaiyo mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo” Alisema Vicky
CDT: UDAKUSPECIAL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!