Sunday, 29 June 2014

BOKO HARAM WASHAMBULIWA NA NYOKA WA AJABU NA NYUKI, WAKIMBIA PORINI


Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria linaelezwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia.

Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi
wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha. Kumezuka hisia za kiimani kuwa Boko Haram wanaadhibiwa na mizimu ya watu waliokuwa waliowauwa kinyama.Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindwa na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!