WATU watatu wameripotiwa kufariki dunia katika matukio tofauti, akiwamo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Pius Msekwa, Salumu Omar (6) aliyegongwa na gari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema jana kuwa mwanafunzi huyo aligongwa na gari T 312 AER Nissan Civilian lililokuwa likiendeshwa na Didas Vedasto (42), alipokuwa akijaribu kuvuka barabara. Dereva anashikiliwa na polisi.
Katika tukio jingine, Gidion Lucian (22), mkazi wa Bunju ‘A’, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari alipojaribu kuruka kutoka katika gari alilokuwemo, akijiokoa baada ya gari hilo kushindwa kupanda mlima na kurudi nyuma.
Wakati huohuo, mwendesha baiskeli January Ngonyani anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema Ngonyani alifariki dunia baada ya kugongwa na gari T 574 AZC lililokuwa likiendeshwa na John Chikoma (37), mkazi wa Ukonga, katika barabara ya Panasonic, Kata ya Chang’ombe.
No comments:
Post a Comment