Tuesday, 13 May 2014

VIDEO JUU YA JAY-Z KUPIGWA NA SHEMEJI YAKE DADA YA BEYONCE SOLANGE

Screen Shot 2014-05-12 at 11.40.31 PMNi video kamili ikionyesha kilichotokea kwenye lifti ambapo rapper Jay Z anaonekana akipigwa na shemeji yake ambae ni Solange kwa muda usiopungua dakika 2 kwa kutumia pochi na mateke na baada ya hapo wakatoka nje ya lift.


Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, haya yalitokea wiki iliyopita kwenye After Party ya Met Gala ndani ya Standard Hotel, NYC na ndani ya video inaonesha Jay Z, Beyonce na Solange wakiingia katika Lifti halafu Solange anaanza kumuwakia Jay z kabla ya kuanza kumvamia wakati huo Beyonce akiwa pembeni tu ametulia na wala haingilii.
Bodyguard aliekuemo katika lifti hiyo alianza kumzuia Solange lakini alifanikiwa kuponyoka kama mara tatu hivi na kuendelea kumpiga Jay Z pia kuna muda Solange alirusha teke na Jay Z akazuia lakini hakurudisha kwa aina yeyote ile, sio kwamba alishindwa kumpiga ili alifanya maamuzi ya kuwa mstaarabu tu.
Screen Shot 2014-05-12 at 10.22.51 PM
Moja kati ya picha za Jay Z na Solange
Beyonce alikua amesimama tu bila kufanya chochote kile ambapo mpaka sasa bado haijulikani sababu ya ugomvi huo ambapo walipofika floor ya 12 bodyguard alibonyeza kitufe cha dharura (emergency button) ili kuficha yanayotokea na kisha baadae
wote watatu walitoka hotelini hapo huku Solange akionekana kukasirika, Beyonce akijaribu kuonyesha smile kwa mbali huku Jay Z akionekana kukasirika kabisa na hata kuwatolea nje mashabiki waliokua wanataka kumbukumbu.
Beyonce na Solange waliingia kwenye gari moja na Jay Z alipelekwa kwenye gari jingine na bodyguard ambapo mpaka sasa chanzo kamili cha ugomvi huo bado hakijajulikana.
Hizi hapa chini ndio video mbili za ilivyotokea ambapo video ya kwanza inawaonyesha wakiwa kwenye lift na video ya pili wakiwa wanatoka nje ya hoteli baada ya ugomvi kutokea.
Screen Shot 2014-05-12 at 10.23.25 PM
Beyonce na Solange





CRD: BET IMETAFSIRIWA NA MILLARDAYO.COM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!