Rais Jakaya Kikwete amesema serikali yake itaendelea na mikakati iliyokwisha anza ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kudhibiti mfumuko wa bei ili nyongeza za mishahara zilete tija na kuwa na maana kwa wafanyakazi.
Mh Kikwete ameyasema hayo katika madhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
Aidha katika hotuba yake Mh Kikwete ametangaza ongezeko la mshahara kwa sekta ya umma sambamba na kupunguza kodi ya wafanyakazi yaani pay as you earn.
Mh Kikwete amewataka waajiri na waajiriwa kuhakisha wanafuata taratibu za kazi na kwamba vitisho na migomo kamwe haviwezi kuleta tija katika sehemu za kazi.
Naye katibu mkuu wa shirikisho la wafanyakazi nchini Bw Nicholas Mgaya akisoma risala ya wafanyakazi amebainisha mambo mbalimbali ambayo kwa kipindi cha karibuni yamekuwa ni kero kwao.
Awali katika maadhimisho hayo Mh Rais alipokea maandamano ya wafanyakazi kutoka katika mashirikia na tasisi mbalimbali pamoja na kutoa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi bora huku veta ikitoa mfanyakazi bora wa kitaifa
No comments:
Post a Comment