Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetenga Sh6 bilioni kukopesha vijana kufanya shughuli za ujasiriamali.
Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Femina Hip ulioshirikisha vijana kutona shule mbalimbali nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Vijana, James Kajugusi alisema fedha hizo zitakopeshwa kwa vijana kupitia vyama vya ushirika vilivyopo halmashauri.
“Tutatoa fedha hizi kupitia Saccos, vikundi vya vijana viainishe mpango kazi wa kujiajiri ambao utatufikia na kuupambanua, tukiona una manufaa kwa taifa basi tutaoa mkopo wenye riba nafuu,” alisema Kajugusi.
Alisema tayari Serikali imepokea zaidi ya maombi 3,000 ambayo wanayapitia ili kutoa mikopo.
Alisema vijana inabidi wajiajiri wenyewe bila kutegemea kuajiriwa kwa kutumia elimu waliyonayo, fursa za maendeleo zinazowazunguka maeneo yao.
“Tanzania tuna idadi ya vijana milioni 16.2 na kila mwaka vijana milioni 2 wanaomba ajira sekta ya umma, lakini ni takriban 100,000 wanaoajiriwa na wengine wanajiajiri wenyeye,” alisema.
Katika mkutano huo, Femina Hip ilizindua logo yake mpya na kutoa zawadi kwa Mwalimu Gaudence Mhando wa Sekondari ya Wasichana ya Iringa, kwa kuchochea maendeleo kwa wanafunzi wake kupitia klabu
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment