Sunday, 11 May 2014

MSIBA WA KADA WA CHADEMA KALOLO, VYAMA VYAWEKA UPINZANI PEMBENI NA KUFANYA MAZISHI YA KIHISTORIA








Waombolezaji

Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard  akichangia
Msafara  wa  kuekea kuzika
Msafara  kuelekea  kuzika
Msafara kuelekea makaburini
Baadhi ya  wadau  wakielekea  kuzika
Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi Chadema akiweka udongo
Ndugu  wakiweka mashada
Ndugu wa kalolo kutoka Kenya  akiweka shada
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas akiweka  shada la maua  katika kaburi la kada maarufu wa Chadema mkoa wa Iringa Gervas Kalolo  wakati wa mazishi  yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Mstahiki meya  Amani Mwamwindi  akiweka  shada la maua
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akiweka shada
 Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiweka  shada la maua  katika kaburi la kada maarufu wa Chadema mkoa wa Iringa Gervas Kalolo wakati wa mazishi  yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
            Na  Francis Godwin Blog

*******
MAZISHI  ya  kada maarufu  wa  chama cha  Demokrasia na maendeleo (Chadema) Gervas Kalolo yatikisa mji  wa Iringa baada  baada ya magari  zaidi ya 100 na boda boda na bajaji  zaidi ya 200 kupamba  msafara  wa mazishi hayo jana

Mazishi  hayo ambayo  yaliongozwa na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa yalionyesha  kuvunja  rekodi ya mazishi  yaliyopata  kufanyika katika mji  wa Iringa .

Awali utaratibu wa mazishi hayo  ulitaka kuvurugika  kutokana na vijana wa Chadema  kuanza kuzomea makaburini  wakati Mc  wa mazishi  hayo wakati  akitambulisha taratibu  za watoa salam  mbali mbali na kumtaka  mwakilishi wa  chama  cha mapinduzi (CCM)  huku akishindwa  kumtaja  mwakilishi wa Chadema na  kuishia  kusema  kutakuwa na mwakilishi wa chama bila kutaja  jina la chama  husika .

Hata  hivyo baada ya MC huyo kufuatwa na diwani  wa Chadema kata ya Mvinjeni  Frank Nyalusi na kumlazimisha  kutaja jina la Chadema badala ya kuishia  kutaja chama bila  jina lake ,ndipo  alipolazimika kuepusha  vurugu kwa kutaja jina la chama cha Chadema na kupelekea  kuibuka kwa shangwe  katika msiba  huo.

Mbali ya  kuibua shangwe kwa  kuimba wimbo  wa Chadema Chadema alisimama mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa ambae  pia alishangiliwa kwa  nyimbo  hizo  za Chadema .

Akizungumza  katika mazishi hayo mbunge Msigwa mbali ya  kumshukuru mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi na viongozi wa CCM kwa  kushirikiana na chama katika mazishi hayo bado  alisema  kuwa kimsingi siasa katika msiba  huwekwa kando.

Mbunge Msigwa  alisema  kuwa  kiongozi  yeyote na mtu  yeyote  mchango wake  hupimwa kwa matendo yake na kuwa umati wa wananchi  waliojitokeza katika mazishi hayo ni wazi  kuwa Kalolo  alikuwa ni kiongozi wa mfano katika jamii na kuwa Chadema itamuenzi kwa kusimamia msimamo  wake wa kupinga ufisadi .

Kwa  upande  wake  mwakilishi wa CCM katika mazishi hayo Shadrack Mkusa  alisema kuwa Kalolo ambae  alipata  kuwa diwani wa kata ya Miyombini Kitanzini kabla ya kushindwa katika  kura za maoni na  kujiunga na Chadema.

Alisema kuwa Kalolo anakumbukwa kwa  mengi ambao amepata  kuyafanya  likiwemo la kusimamia  hoja zake  katika vikao  vya madiwani pamoja na kujitolea  kusaidia  watoto  yatima katika kata  yake.

CHANZO: ALLYSHAMS BLOG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!