Friday, 2 May 2014

MAAMBUKIZI YA VVU NCHINI YAPUNGUA.

Dawa za Kurefusha Maisha ya Waathirika wa Ukimwi ARV
MGANGA Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, amesema maambukizi  ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1988 hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka huu.

Mmbando alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akifunga mradi wa kupunguza maambukizi ya VVU ujulikanao kama Champion.
Alisema katika mradi huo umekuwa na mafanikio kwao kwani walipata fursa za kutoa huduma kwenye mikoa mbalimbali na vijiji 14 vilivyogunduliwa kuwa na maambukizi makubwa.
Alisema mradi huo pia umeweza kutoa elimu katika kamati mbalimbali za Ukimwi kuanzia ngazi ya kitaifa, wilaya, mikoa, kata na mitaa, ili kuhakikisha maambukizi hayo yanapungua au kwisha kabisa.
“Elimu ina umuhimu wake katika jambo hili na kwa kufanya hivi tunaifikia jamii kwa urahisi zaidi,” alisema

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!