WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam, likiwemo la Richard Kijazi kujinyonga akidai amemkumbuka mkewe aliyefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema kuwa mwanaume huyo alikutwa amejinyonga chooni juzi saa 10:00 jioni maeneo ya Kijichi huku akiwa ameacha ujumbe wa maandishi mezani kueleza sababu ya kufanya hivyo.
“Naomba nieleweke wazi kwamba tukio hili hajahusika mtu yeyote, ila nimeamua kufanya hivi kwa kuwa nimemmiss mke wangu, mama John. Naomba nizikwe Dar es Salaam na Mchungaji Haule, na ujumbe huu uheshimiwe,” ulisomeka ujumbe wake.
Kwa mujibu wa kamanda, uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa mwaka 2012, Kijazi aliondokewa na mkewe wa ndoa, mama John kwa ugonjwa wa malaria.
Alisema kuwa tangu wakati huo ndipo tafrani ya kutishia kujinyonga ilianza mara kwa mara, lakini alikuwa akishindwa kutokana na msaada wa karibu katoka kwa ndugu zake.
Katika tukio jingine, Kiondo alithibitisha kutokea kwa ajali ambayo ilisababisha kifo cha Said Jongo (32) mkazi wa Saku, ambaye ni mwendesha bodaboda.
Alisema kuwa juzi saa 10:00 jioni katika barabara ya Chamazi maeneo ya Charambe-Mbagala, gari lenye namba za usajili T 412 ATJ Coaster likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika kutoka Rangi tatu kuelekea Chamazi, aliigonga kwa nyuma pikipiki yenye namba za usajili T 282 CEY na kusababishia kifo cha Jongo.
No comments:
Post a Comment