Tuesday, 29 April 2014

WAZAZI TUCHUNGUZE UHURU TUNAOWAPA WATOTO

Katika mfululizo wa makala za malezi kwa watoto nimekuwa nikisisitiza kuwa ni muhimu watoto wapewe fursa ya kushiriki katika masuala ya kifamilia.
Hata hivyo, ushiriki wao uwe katika kuchangia mawazo kwa yale mambo  yanayowahusu. Pia  nilieleza kuwa uhuru kwa watoto uwe na mipaka.
Kwa mfano, kuna wakati watoto wanaomba ruhusa ya kwenda kucheza na wenzao michezo ya aina mbalimbali.
Haya ni matakwa ya watoto wa rika zote na hivyo tutambue kuwa michezo siyo burudani tu bali pia ni fursa nzuri kwa watoto kuzoeana, kupendana na kujenga urafiki na ustawi. 
Hata hivyo, michezo mingine isiruhusiwe kwani huathiri maadili ya watoto. Kwa mfano, michezo kama  kucheza disko na  kuangalia runinga kwa kipindi kirefu.
Pia kuna mambo  yanayoweza kuathiri maadili yao kama vile kuangalia picha za ngono. Yako mabanda mengi yaliyozagaa mitaani ambayo watoto huangalia picha zenye kupotosha maadili.
Wakati mwingine watoto wanakwenda kwenye nyumba za starehe bila wazazi wao kujua.
Nilipata habari kutoka kwa  familia moja  kuwa watoto  wa umri wa miaka 10  hadi 15 huruhusiwa kwenda ufukweni peke yao bila wazazi kuwafuatilia.
Tabia hii inajengeka hasa wakati wa wikiendi, wakati wa likizo na pia wakati wa sikukuu za dini.  Wako baadhi ya watoto  waliozoea kwenda ufukweni au disko na wakati mwingine hawarejei kabisa nyumbani.
 Watoto  hawa walijenga tabia ya kufanya matendo wachafu ambayo yaliwafanya  warudi nyuma kimasomo. Wa kulaumiwa ni nani kama siyo wazazi? Liko  suala la matumizi ya runinga pamoja na kanda za ngono ambazo watoto wanaazimana. Kanda hizi na hata picha za ngono ziko kwenye intaneti na mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na  Youtube. 
Zinawaharibu  watoto wetu kiasi cha kushindwa kujifunza na kufanya kazi zao za nyumbani (Home work).
Halipo jibu la moja kwa moja lakini tuepuke kuwapa watoto uhuru usiokuwa na mipaka, kwa kuwaacha wafanye wanavyotaka kama kuangalia picha kwenye runinga au mitandao ya kijamii wakiwa sebuleni peke yao
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!