Siku ya Ijumma 4 April 2014 niliripoti kuhusu mabinti wakitanzania walioko nchini China ambao wanatumikishwa kufanya biashara haramu ya ngono na wanaojiita MAMA au BOSS LADY.
Baada ya kuweka audio clips za hao mabiniti wakilalamika na kuomba msaada ndipo nilipo amua kuanzisha campaign ili kuwasaidia mabinti hao walioko MACAU. Nilijaribu kwa hali na mali kutafuta mawasilano ili kujua wako wapi na kama habari hizi ni za ukweli. Nilibahatika kuongea na baadi ya watu wanao ishi huko na wakanihakikishia kwamba habari hizo ni za kweli na walinihakikisha kwamba kuna mabinti wadogo sana wanaotumiwa katika biashara hiyo haramu na wanahitaji msaada haraka iwezekanavyo ingawa wanaogopa kutokana na vitisho wanavyopewa na hao wanaojiita mabosslady au mama zao. Baada ya hapo ndipo harakati za kuwasaidia zilipo anza na kwa kushirikaina na kaka yangu KWAME tukawasiliana na shirkia la IOM (International Organization for Migration) ambao ndo mara nyingi husaidia watu wenye matatizo kama haya kurudi nyumbani wakatushauri cha kufanya so tukawasiliana na police wa MACAU na kuwaelezea tatizo zima na ndipo jana Jumamosi 5 April 2014 walifanikisha zoezi hilo kama inavvyo repotiwa hapa chini kwenye taarifa ya habari ya TDM ENGLISH NEWS ya MACAU:
Natoa wito kwa Serikali kupitia wizara yake husika kuliangalia kwa ukaribu hili suala na kuweza kuwaelimisha mabinti huko nyumbani juu ya mambo haya na athari zake. Yaelekea wengi wanapelekwa nchi za watu bila kuelimishwa vizuri au bila kuwa na ufahamu wa nini haswa wanaweza kukutana nacho huko. Tuna penda kuishukuru Serikali ya Macau kupita jeshi lake la Polisi kwa kuweza kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika wa biashara hii
HABARI ZAIDI KWENYE VIDEO HAPO CHINI....
CHANZO: EMANUEL SHILATU
No comments:
Post a Comment