Saturday, 26 April 2014

TANZANIA YAGONGA MIAKA 50

Wakati leo ni maadhimisho ya  miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa taifa la Tanzania, wasomi, viongozi wa dini, watendaji wa Serikali na wananchi wa kawaida wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu uhai wa Muungano huo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi walitaka Muungano huo uvunjike kwa madai ya kutokuwa na manufaa yoyote, au uwe wa Serikali moja, huku wengine wakitaka uenziwe kwa sababu ndiyo chachu ya amani, umoja na mshikamano uliopo sasa.
Moshi
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St. Augustine, Padri Francis Shawa alisema: “Muungano uendelee ila kuwe na serikali moja kama ilivyokuwa awali na Rais akitoka Zanzibar makamu atoke Bara na kusiwe na marais wawili.”
Alisema  wadhifa wa Rais wa Zanzibar na makamu wake viondolewe na pande zote zikubali baadhi ya vitu kutoa sadaka kwa kuvipoteza.
“Nakerwa  zaidi na Zanzibar kuwa na Katiba yao , wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Zanzibar ni sehemu ya nchi yake pia. Wakati wa Sherehe za Muungano, Rais wa Zanzibar ndiye anaonekana mwenye nguvu, kitu ambacho siyo sahihi. Rais wa Tanzania ndiye apewe hadhi kubwa,” alisema.
Diwani wa Kata ya Kilema Kusini, Kawawa Lubega alipendekeza Serikali mbili na alitoa sababu kuwa hata Serikali mbili za sasa bado wananchi hawajazifahamu vizuri. Lubega alisema kwamba shirikisho la serikali tatu litasababisha Rais atakayekuwapo madarakani akose nguvu kiuchumi na kiutawala.
Ofisa Elimu wa Shule za Sekondari za Wilaya ya Moshi, George Jidamva alipendekeza kuwapo kwa serikali mbili, lakini akashauri Katiba zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar, ziwekwe mezani ili dosari zilizopo zirekebishwe akitaja kipengele cha madaraka ya Rais.
Mwanasheria wa Serikali, Wilaya ya Moshi, Glorian Issagya alipendekeza pia serikali mbili ziendelee, lakini akasema wabunge waliojitoa bungeni, warudi ili changamoto zinazojitokeza ziweze kufanyiwa kazi zisije zikaleta athari hapo mbeleni

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!