MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimezidi kusababisha maafa ambapo jana ukuta wa hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilizopo eneo la Mabibo ulianguka baada ya kuzidiwa na maji na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Mwenyekiti wa Kata ya Makuburi, Moshi Kaftany, aliliambia gazeti hili kwa simu kuwa maafa hayo yalitokea kati ya saa 7:00 na 8:00 mchana ambapo ukuta huo uliangukia nyumba mbili za jirani na kusababisha maafa hayo.
Alisema kuwa ndani ya nyumba moja alikuwemo mfanyakazi wa ndani wa kike ambaye maji yalimfika kifuani na kumzidi nguvu.
Kaftany alifafanua kuwa hadi alipopatiwa msaada wa kutolewa ili kupelekwa hospitali alikuwa tayari amefariki.
“Ukuta wa Mabibo ni mrefu, wapata mita 60 kwenda juu, sasa mvua ilipokuwa kubwa maji yakaongezeka kwa kasi na kuuangusha na hatimaye kusababisha hayo mauaji,” alisema.
Kwa mujibu wa Kaftany, marehemu huyo ambaye hakutambulika jina lake mapema, anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 au 21
No comments:
Post a Comment