UKISEMA wewe unateseka inawezekana hujawaona wanaoteseka. Kijana Peter Andrea (23) mkazi wa Mlandizi, Bagamoyo, Pwani anaishi kwa mateso ya tumbo kuvimba kwa miaka 13 sasa huku akishindwa kusoma na kutekeleza ndoto za maisha yake ya baadaye.
Akizungumza kwa uchungu na Amani kuhusu mateso anayoyapata kwa kipindi chote hicho, Peter alisema matatizo hayo yalianza kumkumba akiwa na miaka 10 tangu kuzaliwa.
Alisema hali hiyo ilianza kwa kila siku akiamka kujikuta amevimba mwili, siku nyingine amevimba uso mpaka akafika hatua tumbo likashika nafasi ya moja kwa moja. “Nilikuwa nikiamka asubuhi najikuta nimevimba mwili, mara uso. Ikafika wakati tumbo nalo likavimba. Nimezunguka kwa madaktari tofauti na mama kipindi akiwa hai kwa bahati nzuri nikapona. Lakini nilikaa kidogo tu hali ikajirudia kama unavyoniona,”
Kijana Peter Andrea akiwa na Baba yake mzazi.
alisema Peter na kuongeza: “Baada ya mama kufariki dunia nikawa naishi maisha ya kuzunguka na kuomba msaada kwa watu bila mafanikio. Mwaka 2013 nilipata msaada kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, akanipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (Dar) ambapo nilifanyiwa vipimo
na kugundulika nina matatizo kwenye ini, nikapewa dawa na kuhudhuria kliniki
“Baada ya vipimo vya mwanzo nilirudia tena kwa mara nyingine, niligundulika pia nina matatizo ya figo, moyo na kibofu cha
mkojo. Niliumia sana, niliia sana. Niliambiwa nikatumie dawa za mitishamba halafu niwe nakwenda kupima lakini nimetumia dawa.
na kugundulika nina matatizo kwenye ini, nikapewa dawa na kuhudhuria kliniki
“Baada ya vipimo vya mwanzo nilirudia tena kwa mara nyingine, niligundulika pia nina matatizo ya figo, moyo na kibofu cha
hizo mpaka sasa sioni dalili yoyote ya kupona.”
Akaendelea: “Ninawaomba Watanzania wenzangu wajitokeze kunisaidia nipone kwani sijabahatika kusoma tangu nikiwa mdogo,
nimejitahidi kusoma elimu ya watu wazima (Memkwa) nimeishia darasa la pili, nawaomba mnisaidie jamani nateseka sana na haya
magonjwa karibu manne.”
ANAHITAJI MSAADA
Kama umeguswa na mateso ya Peter na unahitaji kumsaidia, wasiliana naye kwa simu namba 0716 782 682 au 0659 690 968.

No comments:
Post a Comment