Thursday, 10 April 2014

MPIRA WA VIKAPU WAWILI KWENDA MAREKANI

Dar es Salaam. Wachezaji wawili kati ya watatu wa mpira wa kikapu wanatarajia kuondoka leo kwenda kwenye majaribio katika Chuo cha Post University, Marekani.
Wachezaji hao walipata mwaliko huo kutoka kwa aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya kikapu Mmarekani Albert Sokaitis ambaye pia anafundisha katika chuo hicho kilichopo Connecticut jijini New York.
Wachezaji hao ni Tukusubila Mwalusamba (Vijana Queens) na Rehema Silomba (Don Bosco Lady Lioness) ambao wataongozwa na kocha Robert Manyerere wakati Musa Chacha wa JKT akikwama.
Kabla ya kujiuzulu kufundisha timu hiyo kocha huyo aliahidi kutoa ushirikiano katika Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) ili kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana.
Sokaitis amegharimia dola za Marekani 8,000  (Sh 12.8 milioni) ikiwa ni kwa ajili ya tiketi pamoja na malazi kwa wachezaji hao na kocha atakayeongozana nao.
Kocha Manyerere alisema kuwa Chacha ameshindwa kwa sababu hajafanya majaribio ya kupata Visa. Alisema kuwa TBF nayo imeshindwa kuwalipia Visa wachezaji hao ambapo kila mchezaji alitakiwa kulipiwa Dola 160  (Sh 255,000) kwa kile kilichoelezwa kuwa kwa sasa hawana fedha

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!