Friday, 11 April 2014

MKASI KUPIGA HODI KENYA

Mkasi kupiga hodi Kenya







KIPINDI cha televisheni cha Mkasi kilichoanzishwa na msanii anayefanya muziki na biashara, Ambwene Yessaya ‘AY’,  kinatarajia kupanua wigo wake ikiwemo kufanyikia nchini Kenya.
Kwa mujibu wa AY, akinukuliwa na mtandao mmoja wa Kenya, ameamua kupanua wigo wa kipindi hicho sambamba na kuangalia fursa zaidi anazopata kwa wadau wake.
“Tupo hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu, ambacho kwa sasa kinarushwa katika East Africa TV,” alisema AY.
Hata hivyo, uwepo wa ‘crew’ nzima ya waandaaji wa Mkasi, akiwemo Salama Jabir, Josh Murunga na AY, nchini Kenya, inadhihirisha kuwa tayari wameshaanza mkakati wa kuandaa msimu mpya wa kipindi hicho kuwa na maudhui ya Kenya.
Hivi karibuni katika kipindi cha Mkasi, Salama Jabir  alimhoji AY na moja ya vitu alivyosema ni pamoja na hicho cha kuhamishia kipindi hicho Kenya
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!