Friday, 25 April 2014

INGEKUWA NI WEWE UNGEMFANYAJE HUYU BWANA?




Nilifunga ndoa na mume wangu miaka 20 iliyopita dini ya kiislam. Mungu ametujalia watoto watatu (mmoja wa kiume na 2 wakike.  Mume wangu ni mwalimu wa sekondari kwa miaka 16 sasa na mie mwalimu wa elimu ya msingi kwa miaka  14.


Mie na mume wangu tulihamia nje ya nchi (UK) miaka 8 iliyopita kikazi tukafanikiwa kuhama na watoto 2 mtoto wa tatu tulimzaa UK.TATAZO:
Mwaka 2012 January tuliamua kuanza ujenzi wa nyumba ya kuishi TZ, kwa makubaliano kwamba mie na mume wangu tutakuwa wasimamizi wa ujenzi huo (tusitumie ndugu kusimamia, hofu tutatapeliwa).Tulikuwa na joint bank account kiasi kila mmoja wetu alitumia pesa kwa adabu ili tutimize ndoto zetu za ujenzi na maisha ya baadae.
Mume wangu alikuja TZ kuanza project ya ujenzi, alifanikiwa kumaliza msingi wa nyumba ya vyumba 12. Mara akaniambia amefanikiwa kupata kazi ya afisa utalii Capetown hvyo hataweza kurudi UK kuungana nasi.Bila kujua mume wangu aliamua kufunga ndoa ya serikali kwa siri na mdogo wangu ambayo ilimsaidia kumtafutia passport mdogo wangu kama mkewe  wakahamia CapeTown ambako mume wangu alipata kazi ya kufundisha shule ya msingi na sio afisa utalii. Alikataa tusimtembelee akidai anaenda nje ya nchi kikazi. Muda wa kiaka 2 akitoa sababu tusimtembelee na tusiende likizo TZ bila yeye kuwepo nasi.Mwezi wa kumi na mbili niliamua kwenda likizo TZ na watoto, nikamtumia email kumweleza likizo yetu kwani simu alikuwa hapokei  tena.  Nisitaajabu, majibu ya emaili yangu ni TARAKA kuanzia leo wewe si mke wangu tena.  Nimekuachia watoto ni mali yako, nguo nilizo ziacha UK ni zawadi yako ukipata bwana wa kukuoa mpe avae ili usije nisahau kabisa!


NAHITAJI USHAURI KISHERIA:1.      Kauza kiwanja chenye msigi wa vyumba 12  na viwanja 2 plain (pesa katumia)2.      Katoa pesa yote  ktk joint a/c ni mara tu aliponitumia taraka, bila kujali kuwa watoto wanahitaji school   fees ambayo iko ktk a/c hiyo na mie pia hela yangu.3.      Taraka ni ya email4.      Kamzalisha mdogo wangu watoto mapacha
HITIMISHO:1.      Nianzie wapi kisheria kudai haki yangu?2.       Mwanasheria gani  aweza nisaidia?
Kwa sasa niko TZ nataka nipiganie haki yangu na wanangu.

Wanawake wenzangu, ukiona kwa mwenzio kunawaka moto, kwako Zima moshi usije ukawa moto in future!!!
Asanteni.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!