BILIONEA wa Kimarekani Howard G. Buffett kupitia taasisi yake ametoa msaada zaidi wa kukabiliana na ujangili ikiwemo helkopta pamoja na kusomesha marubani. Msaada huo una thamani ya Shilingi bilioni 3.8.
Awali taasisi hiyo ilinunua helikopta moja aina ya R44 na sasa itakodisha nyingine ya aina hiyo na hivyo kuwezesha kuwapo kwa helkopta nne angani kutokana na serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kununua moja na nyingine inanunuliwa na Mamlaka ya uhifadhi ya Ngorongoro.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka wizara ya Maliasili na Utalii ,ufadhili wa bilionea huo kwa sasa umefikia sh. 8,577,060,000 ikiwemo Mafunzoya Marubani ,Kujenga Mabweni Kwa ajili ya wanafunzi 300,Jiko la Kisasa na Karakana.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri Lazalo Nyalandu inaeleza kuwa pia kuna Ujenzi wa Miundombinu ya kuvuna maji ya mvua,ununuzi wa Mabasi aina ya Scania mawili na Malori aina ya Scania mawili pamoja na mafunzo na Mradi wa kuhifadhi Duma .
Alisema helkopta iliyonunuliwa ni kwa ajili Pori la Akiba la Selous ambayo inatarajiwa kuwasili nchini ndani ya kipindi cha miezi 6 kuanzia sasa.
Alisema helikopta iliyokodiwa na taasisi hiyo,itafanya ulinzi wa doria chini ya Mkurugenzi wa Wanyama pori katika Pori la Akiba la Selous kuanzia katikati ya mwezi Mei, mwaka huu wakati zikisubiri helikopta zilizoagizwa toka viwandani nchini Marekani. “
Helikopta hii itatumika kwa miezi sita kuanzia siku itakayowasili nchini, Taasisi hii itagharimia gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za kuikodi ndege, marubani, na mafuta, huku Wizara ikigharamia malazi na chakula cha marubani hao wakiwa katika shughuliza doria hapa nchini”
Alisema Aidha taasisi hiyo ikishirikiana na Wizara imepata wataalamu elekezi wawili,watakao toa ushauri wakitaalamu katika maeneo ya Pori la Akiba la Selous na Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori – Pasiansi kwa muda wamiezi 6 kwa gharama zake huku ikigharamia malazi na usafiri wakiwa nchini.
Nyalandu alisema Serikali kupitia Tume ya ajira imetangaza nafasi za ajira 450 kwa askari wawanyamapori, ikiwa ni sehemu ya jumla ya askari 950 ambao wanategemea kuajiriwa kwa mwaka huu wa fedha.
Pia , Wizara itakipatia Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori – Pasiansi silaha 25, aina ya AK47 kwa ajili ya kuimarisha mafunzo kwa wakurufunzi
HABARI LEO:
HABARI LEO:
No comments:
Post a Comment