Sunday 13 April 2014

ASIA IDAROUS KUFANYA MAONYESHO NIGERIA

Asia Idarous kufanya maonesho Nigeria
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous, anatarajiwa kufanya onesho la mavazi ya ubunifu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, litakalofanyika Abuja, Nigeria, Aprili 25.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, alisema onesho hilo limeandaliwa na umoja wa Watanzania waishio nchini Nigeria, ambapo usiku wa Aprili 25, watakutana kwa pamoja na kufurahia miaka 50 ya Muungano, sambamba na tafrija hiyo ya kipekee itakayowakutanisha magwiji wengine wa ubunifu wa nchi hiyo.
“Nimefurahia sana kufanya onesho nchini Nigeria, bila shaka nitafanya vizuri, kwani nina kila aina ya ubunifu wa mavazi likiwemo  vazi la khanga na mavazi mengine,” alisema Idarous na kuongeza kuwa kufanya onesho hilo nchini humo, ni faraja kwake, kwani nchi hiyo kwa sasa imekuwa ndiyo nchi tajiri katika bara la Afrika, kutokana na uchumi wake kukua maradufu huku ikiipiku Afrika Kusini iliyokuwa ikishikirla nafasi ya juu katika uchumi.
Aliwataka Watanzania hasa wabunifu wa mitindo na wasanii, kubadilika kwa kujikita katika kufanya kazi zenye tija kwa ukuaji wa uchumi kama walivyofanikiwa Wanigeria.
Idarous ama Mama wa Mitindo, ni mkongwe wa mitindo hapa nchini, ambapo amekuwa akiandaa maonesho mbalimbali ikiwemo ‘Usiku wa Khanga za Kale’ na l‘Red in Lady’ kila mwaka nchini

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!