Wednesday, 30 April 2014

ALIYEPIGWA NA CHID BENZ MAHUTUTI!

MREMBO Mwanaisha Kiboye, mkazi wa Ilala, Dar anayedaiwa kupigwa na mwanamuziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, hali imekuwa mbaya kwani yu mahututi.
Mwanaisha Kiboye, akiwa hoi hospitali baada ya kipigo kutoka kwa msanii Chid Benz.
Juzi Jumatatu, wakati staa huyo akipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kwa kesi hiyo, Mwanaisha alikuwa akipumua kwa tabu kwenye chumba maalum katika Hospitali iitwayo Aviation iliyopo maeneo hayo ya Ilala.


MAMA MDOGO ANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mama mdogo wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, hali ya mgonjwa imekuwa tete kwani kwa siku moja amekuwa akizimia zaidi ya mara tano.
Mtuhumiwa Chid Benz.
AZIMIA MARA TANO
“Mwanangu hali yake ni mbaya anazimia zaidi ya mara tano kwa siku halafu watu wananiambia nitoe kesi mahakamani si nitaonekana chizi jamani?” alisema mama huyo huku akilengwalengwa na machozi.
Alisema hali ya mgonjwa imekuwa ikibadilika hasa suala la presha kupanda na kushuka huku mapigo ya moyo yakiwa chini hivyo kuwatia hofu ndugu, jamaa na marafiki.
KIPIMO CHA KICHWA
Aliongeza kuwa siku hiyo (Jumatatu) madaktari na wauguzi walikuwa katika harakati za kumpeleka kwenye kipimo kiitwacho CT Scanning kuangalia madhara yaliyompata kichwani na kusababisha hali kuzidi kuwa mbaya.
Mwanaisha Kiboye akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Aviation, IIala.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuingia wodini ambapo katika kipindi cha saa kadhaa Mwanaisha hakugeuka wala kuamka kutoka usingizini.
TURUDI KWENYE KESI
Juzi (Jumatatu) Chid alitakiwa kupandishwa kizimbani Mahakama ya Mwanzo, Wilaya ya Ilala, Dar kwa ajili ya kesi hiyo lakini hakutokea kortini badala yake alimtuma mdhamini wake amuombee udhuru kuwa alikuwa akiumwa.
CHEMBA KIDOGO
Karani wa mahakama hiyo, Nusura Seleman alipoita kesi hiyo, mdhamini huyo na ndugu wa Chid Benz na ndugu wa Mwanaisha, walijongea kwenye ‘chemba kidogo’ mbele ya Hakimu Leonia Muta.
HAIWEZEKANI
Katika kesi hiyo ambayo mwanahabari wetu aliifuatilia hatua kwa hatua, hakimu Muta aliwaita wenye kesi hiyo lakini wote hawakuwepo ndipo hakimu huyo akasema hawezi kuendelea na kesi hiyo bila wenye kesi wote kuwepo. Shauri hilo liliahirishwa hadi Mei 5, mwaka huu.
MAMA CHID ATOLEWA NDUKI
Akizungumza nje ya mahakama hiyo, kaka wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina la Swedy alisema:
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya namna ile halafu wanatuambia tukayamalize nyumbani, hilo si jambo la kushangaza jamani?
Mama yake Chid Benz alikuja nyumbani kutaka kumuona mgonjwa tukamtoa nduki.
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya hivyo asijekudhurika na jambo lolote akiwa nyumbani kwetu ikaonekana tumemfanyia kusudi.
CHID NAYE ATOLEWA BARU
“Hata Chid Benz mwenyewe naye juzi (Jumamosi iliyopita) alikuja na kutupigia magoti naye tukamtoa baru, asitulee zake kwanza hii siyo mara ya kwanza kumpiga dada yangu kuna kipindi alimpiga kesi ilikuwa Kituo cha Polisi cha Kilwa Road.”
BADO HALI TETE
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni Jumatatu jioni, bado hali ya Mwanaisha bado ilikuwa ni tete.
Chid Benz alidaiwa kumpiga Mwanaisha Siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu maeneo ya Ilala, Dar.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!