Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni kwenye mapishi mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu kwa mbali.Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama viungo jikoni.
Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini chuma(iron),Calcium na Magnesium
Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa mengi.Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata hivyo,tafiti za kisayansi za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi
Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi maana yake ni kwamba chakula hicho kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.
Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :
- Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza tumbo na huondoa gesi kwenye utumbo mwembamba ambayo mara nyingi husababishwa na vyakula tunavyokula hivyo hupunguza utoaji gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana
- Inazuia magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria aina ya Salmonella.moja ya magonjwa haya ni kuumwa tumbo na kuhara.
- Inazuia Ugonjwa wa UTI.Yaani Urinary tract infection
- Inazui kutapika na hali ya kuvurugika tumbo
- Inaondoa gesi tumboni
- Inashusha sukari kwenye damu.(lower blood sugar)
- Inapunguza cholesterol mbaya mwilin
- Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)
- Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito
- Inaondoa maumivu,muwasho,na uvumbe (anti inflammatory)
- Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi
Unaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili kuitumia kama dawa
- Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za giligiliani na maji vikombe viwili.Chuja kisha ongeza sukari kidogo.Kunywa ikiwa yamoto au vuguvugu
- Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha kijiko kimoja cha chai cha mbegu za giligiliani zilizosagwa na maji kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa ikiwa vuguvugu
- Kushusha sukari na kushusha cholesterol.Kunywa chai ya giligiliani (mbegu) mara kwa mara,pia tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye chakula.
- Ili kuondoa chunusi na madoa meusi.Twanga au sigina majani ya giligiliani,chuja au kamua ili kupata maji yake.Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani kisha changanya na kijiko 1 cha chakula cha manjano(Binzari manjano).pakaa kwenye ngozi ,acha ikauke kisha osha au nawa na maji vuguvugu.Onyo:usisugue ngozi
- Kutibu kuhara damu (dysentery).Changanya vijiko 2 vya chai vya maji ya giligiliani na kikombe kimoja cha maziwa fresh ambayo hayajatolewa krim
- Chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza asidi tumboni
Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula ambavyo ni tiba huupa mwili nafasi nzuri ya kuvuna virutubisho na kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.
Ni vyema kujua kwamba asilimia kubwa ya vyakula na viungo tulivyonavyo majumbani ni tiba ya magonjwa mbalimbali.Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia hutokana na mimea,virutubisho huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na kuchanganywa na Kemikali ili kutoa vidonge na madawa ya magonjwA mbalimbali.
No comments:
Post a Comment