Sunday, 2 March 2014

WAZIRI KAWAMBWA AKERWA NA DARAJA LA TANO KUITWA SIFURI.

Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma


Dodoma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa sifuri.


Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alivishutumu vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.
Alisema kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.
“Ndugu zangu waandishi wa habari na paparazi, kitu ambacho hamkufanya haki kwa Watanzania safari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja sifuri,” alisema na kuongeza:
“Unakuaje na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne lakini unapofika la tano unaita sifuri katika namna ambavyo waandishi wa habari walipenda.”

Dk Kawambwa alisema vyombo vya habari vimekuwa vikipenda taswira ya nchi ionekane kuwa ni kufeli. “Lakini ninachosema ni kwamba, pointi ni zile zile tulichoondoa ni daraja la tano.”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!