WATANZANIA 15 waliohukumiwa kunyongwa nchini China baada ya kupatikana na kosa la kujihusisha na dawa za kulevya, wamemsononesha Mkurugenzi wa Kampuni ya 5 Effects Movies Ltd, William Mtitu kwa kile alichosema walikosa elimu ya kina juu ya madhara ya biashara hiyo haramu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mtitu alisema amekuwa akitumia muda mwingi kuangalia namna ya kuwasiliana na watu wanaofanya biashara hiyo ili waachane nayo, lakini anashindwa na njia pekee ambayo imekuwa nyepesi kwake, ni ile ya kutumia filamu kama alivyofanya kwenye kazi yake mpya ya ‘Mr. Kadamanja’, ambayo inazungumzia madhara ya biashara hiyo.
“Hakika baada ya kusikia habari za Watanzania wenzangu kuhukumiwa kunyongwa, machozi yalinitoka, kwani nimekuwa nikitumia muda mwingi kuangalia namna ya kuwafikishia ujumbe watu wanaofanya biashara hiyo nashindwa, ila nikaona njia nyepesi ni kutumia sinema na hivi karibuni nitaiingiza sokoni filamu ya ‘Mr. Kadamanja’, ambayo inaelezea madhara ya kazi hiyo,” alisema Mtitu.
CRD:TANZANIA DAIMA.
HABARI KAMILI KUHUSU KUNYONGWA KWA WATANZANIA 15 NCHINI CHINA HII HAPA CHINI..
CRD:TANZANIA DAIMA.
HABARI KAMILI KUHUSU KUNYONGWA KWA WATANZANIA 15 NCHINI CHINA HII HAPA CHINI..
No comments:
Post a Comment