Tuesday, 4 March 2014

SASA SIO STORI TENA HATIMAYE DARAJA LA KIGAMBONI SI NDOTO TENA CHEKI HAPA


Daraja la Kigamboni limekamilika kwa zaidi ya asilimia arobaini na tano na matumaini
 makubwa
 ya kumalizika kwa ujenzi huo kwa wmuda uliopangwa Julai mwakani yakionekana
 huku nyumba zilizokuwa
 zinazuia ujenzi 
huko zikibomolewa kwa nguvu na serikali.

 
Akizungumza jijini Dar es Salaam meneja mradi huo
injinia Karim Mattaka amesema ujenzi huo umeshaanza kuleta
 matumaini makubwa
 kutokana na nguzo mbili zilizokuwa zinakwamisha kuwa tayari na zoezi linaloendelea
 ni kuhamisha
 maji katika maeneo yalinayochimbiwa nguzo hizo sambamba na kuchimbia nguzo kubwa
 za kupokea
 baraja hilo upande wa barabara ya Mandela.
 
Aidha injinia Karimu amejaribu kufafanua mfumo wa barabara na daraja hilo namna
 utakavyotumika
 baada ya kukamilika na kuwahakikishia watanzania ujenzi huo utakamilika kwa
 wakata kama
 mambo yataenda kama yalivyopangwa.
Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Vijibweni Bw. Athman Ally akielezea kuhusiana na hatua 
iliyochukuliwa
 na serikali ya kuvunja nyumba za baadhi ya wakazi waliogomea fidia amesema wao
 walipewa taarifa
 na mwanasheria mkuu na baadaye akatakiwa kwenda kusimamia zoezi la uvunjaji
 wa nyumba hizo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!