Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na Wananchi wakazi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 wakati wa Muendelezo wa Kampeni zake za kuomba ridhaa kwa Wananchi hao ya kuwa kiongozi wao kwa Maendeleo ya Jimbo la Chalinze.
Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi akiwasisitiza Wananchi wa Kijiji cha Chahua kuzitunza vyema Shahada zao za kupigia kura,ili siku ikifika ya kupiga kura wasipate shida na waweze kupiga kura Mtu anaefaa kuwa Kiongoizi wa Jimbo la Chalinze.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia na kutoa Sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chahua,Christina Kejeli (kulia) akitoa maelezo ya Maendeleo ya Kijiji kwa Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) wakati wa muendelezo wa Mikutano ya Kampeni iliyofanyika leo Machi 27, 2014 katika vijiji vya Chahua na Matuli,Kata ya Bwilingu.
Diwani wa Kata ya Bwilingu,Ahmed Kalama akisisitiza jambo wakati wa kuzungumzia mafanikio ya Kata yake pamoja na Changamoto ambazo bado hazijafanyiwa kazi ndani ya Kata hiyo,mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwasalimia wakina Mama wa jamii ya watu Wafugaji (Wamasai) wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Matuli kwa ajili ya kuendelea na Mikutano ya Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.Picha zote na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment