Mtambo wa Satelite nchini Thailand umenasa picha za mabaki 300 yanayodhaniwa kuwa ya ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea wiki tatu zilizopita.
Picha hizo zilinaswa tarehe 24 mwezi Machi, Siku moja baada ya mtambo wa Satelite wa Ufaransa kunasa picha zengine za mabaki 122 yaliyodhaniwa kuwa ya ndege hiyo.
Aidha picha hizo za Thailand, zinasemekana kuonyesha vifaa 300 vikielea baharini vikiwa vimetapakaa katika eneo lililo umbali wa kilomita 2,700 Kusini Magharibi mwa Perth.
Ndege MH370, ilitoweka tarehe 8 mwezi Machi, ikiwa na watu 239.
Serikali ya Malaysia iliwaambia jamaa na familia za abiria wa ndege hiyo kuwa ilianguka baharini na hapakuwa na manusura wowote
Hakuna taarifa rasmi za mabaki hayo kuonekana baharini.
Msako ulifanywa kwa kutumia ndege na meli ingawa shughuli hiyo ilisotishwa nchinio Australia, Alhamisi kutokana na hali mbaya ya hewa.
Hata hivyo meli nchini Australia zinaendelea na shughuli hiyo licha ya hali kuwa mbaya.
Duru zinasema kuwa picha hizo zimekabidhiwa kwa serikali ya Malaysia hasa maafisa waliokuwa wanaendesha shughuli ya kuitafuta ndege hiyo.
Hata hivyo vifaa hivyo havijathibitishwa ikiwa ni mabaki ya ndege ya Malaysia iliyotoweka
BBC.
No comments:
Post a Comment