Thursday, 13 March 2014

MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA, AFYA NA MAZINGIRA WAZINDULIWA JIJINI DSM

????????Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Enjinia Bashir Mrindoko (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi Uzinduzi wa maji safi na salama Afya na Mazingra (wakwanza kushoto), Balozi wa Ubelgiji Nchini Tanzania Koenraad Adam, na anaefuatia mwenye shati la bluu Mwakilishi wa Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU), Eric Beaume (wakwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Maendeleo Ubelgiji, Peter Moors.

????????Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Enjinia Bashir Mrindoko akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa eneo hilo mara baada ya kuzindua.????????Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu wakiwa na mabango  yenye ujumbe wa maji na mazingra wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo.????????Kikundi cha ngoma Makonde Dansi kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa maji safi na salama Afya na Mazingra.

WANANCHI wa Mbagala Kuu wameilalamikia Shirika la Umeme Tanzania Tanesco kutokana na uzalishaji mdogo wa umeme unaosababisha visima vya maji kushindwa kuzalisha maji  ya kutosha.
Akisoma risala ya wananchi Lydia Changula alisema tatizo la maji safi na salama limeweza kutatuliwa kwa asilimia 100,kikwazo kikubwa ni umeme mdogo unaosababisha kuzalisha maji  chini kiwango.
Alisema mradi wa maji safi na salama,Afya na Mazingira  umesaidia kuwepo kwa tenki za maji 16 ambazo zimesambazwa katika vituo 381 vinavyotoa huduma ya maji safi na salama kwa  watu laki moja na sabiini elfu.
“ Mradi huu umesaidia ujenzi wa   vyoo 21 kwa shule za msingi vyenye matundu 138 na kufanikiwa kukarabati matundu 8 hali iliyosaidia kupatikania kwa huduma bora za vyoo”alisema Changula.
Akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe katibu Mkuu wa wizara hiyo  Enjinia Bashir  Mrindoko alisema mradi huo umetumia zaidi ya bilioni 15 ambazo zimetumika kwa miradi 15 katika manispaa tatu.
Alisema fedha hizo zilitolewa kwa ushirikiano wa nchi ya Tanzania,umoja wa Europe pamoja na ubelgiji ambapo lengo kubwa la kutekeleza mradi huo ni kuweza kupunguza kero ya maji nchi hususani kwa mama na mtoto.
“Malengo ya serikali ni kuhakikisha kero ya maji nchini inapungua kama sio kumaliza kabisa hadi kufikia mwaka 2015 na kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama”,alisema  Mrindoko.
Alisema mradi huo wa maji utasaidia wananchi wanaokaa pembezoni mwa Dar es saalam kwa asilimia 55 na kusisitiza kuwa mradi huo ni zaidi ya matumizi ya wizara lazima itunzwe.
Alisema serikali haitarajii kuona wananchi wanawaachia wajanja kujiunganishia maji hayo kiholela huku matatizo ya maji yakiongozeka badala yake watumie sheria zinazofaa ili kuweza kuunganishiwa maji.
Akisoma hutuba kwa wananchi Balozi wa Ubelgiji Koenraad Adam alisema mradi huo wa maji ni sehemu kuu kwa nchi ya Tanzania na Ubelgiji.
Alisema bila ya maji safi na salama katika taifa hakuna maisha na kuwataka wananchi wasidanganywe na wajanja wachache watakaotumia maji vibaya.
“Mimi ni raia wa ubelgiji licha ya kwamba nchi yangu ni ndogo sana lakini miongoni mwa vitu tulivyobarikiwa ni maji na ndio maana na sisitiza matumizi ya maji yatumike kwa uangalifu,musisubiri kila kitu kufanyiwa na serikali lazima na nyinyi nwenye mubadilike”,alisema Adam
PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!