Saturday, 29 March 2014

MAJANGILI YAFANYA KUFURU HIFADHI YA WAMI MBIKI

Wanyamapori wakiwamo tembo katika Hifadhi ya Wami Mbiki wapo hatarini kutoweka, kutokana na kasi ya vitendo vya ujangili.
Mbali ya ujangili wa wanyamapori, pia ukataji miti kwa ajili ya uchomaji mkaa, na ufugaji wa mifugo ndani ya eneo hilo, ni vitendo vinavyozidi kuongezeka na kutishia kutoweka kwa hifadhi hiyo.
Eneo hilo linaundwa na vijiji 24, wilaya tatu za mikoa ya Morogoro na Pwani, ambapo vijiji vitatu viko Wilaya ya Morogoro, Mvomero vijiji(8), 13 ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, liko kati ya Morogoro, Chalinze, Mbewe, Kanga, Turiani na Wami Dakawa.
Wilaya ya Morogoro, Mvomero vijiji(8), 13 ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, liko kati ya Morogoro, Chalinze, Mbewe, Kanga, Turiani na Wami Dakawa.
Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa ujangili wa wanyama katika hifadhi hiyo huendeshwa kwa kutumia magari, pikipiki, mbwa, mitego ambayo husambazwa eneo kubwa, huku bunduki aina ya gobori na za kivita zikitumiwa kwa ajili kuua wanyama wakubwa kama vile tembo.
Gazeti hili limebaini kuwa wanyama kama simba, chui na mbwa mwitu huuawa kwa sumu ili kukinga mifugo iliyohamishiwa ndani ya eneo hilo isiliwe, huku tembo wakiuawa kwa bunduki na sumu ili kupata meno yake.
Kutokana na kuwapo kasi kubwa ya ujangili na uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo, idadi ya wanyama inapungua kwa kasi.
Taarifa ya watafiti ya mwaka jana kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Teps, inaeleza kuwa hali hiyo ilianza kuwa mbaya zaidi kwa kipindi cha 2010-2013 baada ya kukosa ufadhili kutoka nje na kwamba hata mikataba ya wafanyakazi wa hifadhi hiyo iliisha mwaka 2010 na kukosekana kwa doria.
Pamoja na malori kusomba tani za mkaa kutoka ndani ya pori hilo, hakuna hatua zinazochukuliwa na uongozi wa halmashauri na wizara husika.
Inakadiriwa wanyama zaidi ya 15,000 wamehama ama kuwindwa kwa kipindi cha miaka miwili na eneo limegeuzwa kuwa ranchi ya mifugo na kulimwa ekari za maelfu ya mazao ya mahindi na mpunga ndani ya hifadhi.
MWANANCHI..

Dk. Alfred Kikot

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!