Mcheza sinema maarufu Lupita Nyong’o ambaye ni raia wa Kenya, Jumapili ameshinda tuzo la kifahari la Oscar huko Hollywood California.
Lupita alipata tuzo hilo kwa kuwa muigizaji msaidizi bora zaidi kwenye filamu iitwayo“12 years A Slave”.
Baada ya kupokea tuzo hilo, Lupita alitoa hotuba yenye hisia kali na kuwashukuru wote waliomwezesha kushinda tuzo hilo la Oscar.
Awali macho ya dunia kwa wapenzi wa filam yalielekezwa huko Hollywood kutizama tuzo za mwaka wa 86 za Oscar zikitunukiwa wasanii mbali mbali wa filam duniani.
Kwa upande wa Afrika mcheza filamu mwingine wa mara ya kwanza Barkhad Abdi ambaye ni raia wa Somalia aliteuliwa kuwania katika nafasi ya waigizaji wasaidizi ambapo alishiriki katika filamu “Captain Phillips” ambapo muigizaji Jared Leto alipata ushindi.
Vyombo vya habari vya Kenya viliripoti kuwa wakenya na waafrika kwa jumla walikuwa wakisubiri kuona ikiwa muigizaji Lupita Nyong’o atapata tuzo hilo. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia alikuwa ametuma salamu za kumtakia ushindi Lupita ,katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook.
CHANZO:VOASWAHILI.COM
CHANZO:VOASWAHILI.COM
No comments:
Post a Comment