Mwigizaji nyota wa filamu za kiswahili nchini, Elizabert Michael ‘Lulu’ ametajwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaonogesha uzinduzi wa tamasha la mfuko maalum utakaojulikana kama ”Kanumba The Great Foundation” linalotarajiwa kufanyika April 7, mwaka huu kwenye kiota cha burudani ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala.
Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya Vannedrick, George wakuganda alisema Lulu amekubali kushiriki na tamasha hilo litafanyika siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha marehemu Steven Kanumba.
”Lulu amekubali kuungana na wasanii wenzake katika tamasha hilo kubwa ambalo litakuwa ni mara ya kwanza kufanyika tangu kifo cha Kanumba ”. alisema Wakuganda.
Aliongezea kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na kabla ya siku hiyo, Jumamosi ya Aprili 5 kutakuwa na zoezi la wasanii kutembelea hospitali , magereza, vituo vya watoto yatima na kaburi la marehemu Kanumba.
No comments:
Post a Comment